HabariMilele FmSwahili

Waziri Chelugui: Serikali imebuni mkakati mwafaka wa kusimamia raslimali za maji nchini

Serikali imebuni mkakati mwafaka wa kusimamia raslimali za maji nchini. Waziri wa maji Simon Chelugui anasema mkakati huo unajumuisha ujenzi wa mabwawa makubwa 57 likiwemo la Thwake kaunti ya Makueni. Ameelezea imani kuwa mpango huo utasaidia pia katika kukabili uhaba wa maji unaoshuhudiwa hapa jijini kutokana na kupungua kwa kiwango cha maji katika bwawa la Ndakaini. Amewataka wanasiasa kutowachochea wenyeji kutakako tekelezwa miradi hiyo kuipinga.

Show More

Related Articles