HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa EALA Simon Mbugua ashtakiwa kwa tuhuma za wizi wa kimabavu

Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki EALA Simon ameshitakiwa kwa tuhuma za wizi wa kimabavu. Mbugua pamoja na washukiwa wenguine wawili wanadaiwa kumvamia na kumwibia aliyekuwa mwenyekiti wa wafanyibiashara wa kati kati ya jiji la Nairobi Timothy Muriuki shilingi laki moja. aidha wanadaiwa kumjeruhi Muriki katika hoteli moja hapa jijini Nairobi mnamo tarehe 30 mwezi ulioita. Washukiwa wengine ni Antony Otieno Ombok na Benjamin Odhiambo Onyango. Wote wamekanusha mashitaka. kupitia wakili Nelson Havi wameitaka mahakama kuwaachilia kwa dhamana. Hakimu mkuu Martha Mutuku atatoa uamuzi saa nane mchana kuhusu iwapo wataachiliwa kwa dhamana au la.

Show More

Related Articles