HabariPilipili FmPilipili FM News

Hofu Ya Ongezeko La Visa Vya Dhulma Za Kijinsia Ya Tanda Katika Kambi Za Waathiriwa Wa Mafuriko, Kilifi.

Siku chache baada ya serikali ya kaunti ya Kilifi kusambaza zaidi ya mipira ya kinga 3,000 katika  kambi za waathiriwa wa mafuriko huko garashi eneo bunge la Magarini, washikadau wa masuala ya watoto sasa wameeleza wasiwasi wao juu ya hofu ya ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia dhidi ya watoto katika kambi hizo.

Akizungumza na wanahabari afisa wa watoto katika shirika la kutetea haki za watoto la Kesho mjini Kilifi Hedaya Chunge amesema kuna hofu kubwa kwa wanaume wengi katika kambi hizo kutumia fursa hiyo vibaya na kushiriki ngono  kiholela na wasichana wa umri mdogo.

Show More

Related Articles