HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mjumbe wa EALA Simon Mbugua akamatwa kwa kumdhalilisha mkuu wa NCBDA

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Simon Mbugua na watu wengine watatu wamekamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Central hapa jijini Nairobi.
Hii ni kufuatia vurumai na kudhalilishwa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wafanyibiashara wa kati kati mwa jiji Timothy Muriuki aliyepigwa na kuumizwa na wahuni katika hoteli moja hapa jijini, juma lililopita.
Baada ya mbunge huyo kuandikisha taarifa alichukuliwa na makachero kwa uchunguzi zaidi huku polisi wakitilia mkazo kuwa bado wanaendeleza uchunguzi na jitihada za kuwakamata washukiwa wengine zi mbioni.

Show More

Related Articles