HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Mama aliyeokolewa na wanawe asizame Murang’a azungumza

Wahenga walisema uchungu wa mwana aujuae ni mzazi lakini je, kinyume cha msemo huu huwa ni nini? Poromoko la ardhi katika eneo la Gitugi kaunti ya Murang’a lililosababisha vifo vya watu wanne limedhihirisha utu na ushujaa wa watoto wawili walio chini ya umri wa miaka kumi baada ya wao kuhatarisha maisha yao na kuyaokoa maisha ya mama yao aliyekuwa amekwama kwenye tope.
Usiku huo wa ijumaa ni usiku ambao kamwe wakazi wa Gitugi hawatausahau kwani kulingana nao ulikuwa ni kama siku ya kiama!

Show More

Related Articles