HabariMilele FmSwahili

Matiangi’ aamuru kufunguliwa upya faili ya mauaji dhidi ya kasisi Ng’ang’a

Waziri wa usalama wa kitaifa dr Fred Matiangi ameamuru kufunguliwa upya faili ya uchunguzi wa kesi iliomkabili kasisi wa kanisa la Neno Evangelism James Ng’ang’a. Matiangi anasema hajaridhishwa na uamuzi wa mahakama kumuachilia huru nganga licha ya kuwepo ushahidi wa kutosha kumhusisha na mauaji ya mama mmoja miaka 3 iliyopita baada ya kumgonga kwa gari lake. Kadhalika Matiangi ameishurutisha afisi ya jinai kuendesha uchunguzi wa kina kwa lengo la kuishauri tume ya huduma za mahakama kuhusiana na hatua bora za kuchukua dhidi ya walioafikia uamuzi wa kuamuachilia huru Nganga. Askofu huyo aliachiliwa huru pamoja na dereva wake Simon Kuria na afisa wa polisi Christopher Nzioka, uamuzi uliotolewa na hakimu mkaazi wa mahakama ya Limuru Godfrey Oduor.

Show More

Related Articles