HabariMilele FmSwahili

Miili ya watu wanne yapatikana mto Enziu, Kitui

Miili minne ya watu waliozama mto Enziu kaunti ya Kitui baada ya kusomba na mafuriko imepatikana majuma 3 baadaye. Maafisa kutoka shirika la msalaba mwekundi na mashirika mengine ya uwokozi wameokoa miili hiyo ambayo ilizama pamoja gari lao aina ya Probox. Mabaki ya gari hilo pia yamefukuliwa kutoka kwa mto huo
Wakati huo serikali ya Makueni imetangaza hivi karibuni itazindua mfumo wa teknolojia ambapo wenyeji watakuwa wanajulishwa kupitia simu za rununu kuhusu hali ya hewa eneo hilo. Waziri wa mazingira Makueni Mary Mbenge anasema kupitia mfumo huo, itakuwa rahisi kuwatahadharisha wenyeji dhidi ya kujiopata maeneo hatari hasaa msimu huu wa mvua

Show More

Related Articles