HabariMilele FmSwahili

Takriban watoto laki 800 Nairobi kupokea chanjo ya polio kuanzia kesho

Takriban watoto laki 800 waliochini ya miaka 5 hapa Nairobi watapokea chanjo ya polio zoezi linaloanza kesho hadi jumapili hii. Kima cha shilingi milioni 100 kikilengwa kutumika katika zoezi hilo la siku 5, linalowadia baada ya mkurupuko wa polio type 2 iliyoripotiwa maeneo ya Kamukunji na Eastleigh. Wakati huo shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa dola nusu milioni kufadhili kampeni za kukabiliana na ugonjwa wa polio type 2 humu nchini

Takwimu kutoka idara ya kudhibiti virusi vya polio zinaonyesha nusu ya kaunti nchini hazijaafikia idadi lengwa ya watoto waliopewa chanjo ya polio, Nairobi ikongoza kwa kaunti 5 zilizoathirika zaidi. Ni kutokana na hilo, serikali kupitia wizara ya afya imezindua zoezi la kuwapa chanjo watoto waliochini ya miaka 5 kuanzia kesho hadi Jumapili hii.

Mkuu wa kitengo cha huduma za afya Dr Jackson Kioko anasema mitaa ya mabadana ndio italengwa baada ya mkurupuko wa polio type 2 kuripiotiwa eastleigh na kamukunji. Akizundua rasmi zoezi, Kioko anasema wizara ya afya pia imewatuma maafisa kuwakagua watoto kwenye kambi na mpakani hasaa wa Kenya na Somalia

Show More

Related Articles