HabariMilele FmSwahili

Wakaazi wa Rongai waandamana kulalamikia hali duni ya miundo msingi eneo hilo

Wakazi wa Rongai wanaandaa maandamano hapa jijini Nairobi wakati huu kulalamikia miundo msingi duni ya bara bara eneo hilo. Wakazi hao wananuia kuandamana hadi katika daraja la Fatima ambako watu zaidi ya saba wamefariki katika siku kadhaa zilizopita kutokana na athari za mvua na mafuriko. Mwenyekiti wa wakazi hao Fred Gori anasema watawasilisha ombi lao kwa mbunge wa eneo hilo Joseph Manje na gavana, Kajiado Joseph Ole Lenku na waziri wa uchukuzi James Macharia kuangazia tatizo hilo.

Show More

Related Articles