HabariPilipili FmPilipili FM News

Tahadhari Ya Mvua Kubwa Yatolewa Pwani.

Mvua kubwa inatarajiwa kuendelea kunyesha hadi mwishoni mwa juma hili kwa mujibu wa ripoti ya sasa ya idara ya utabiri wa hali ya hewa.

Ripoti hiyo inaashiria kuwa kaunti zote za pwani zitapokea mvua ya hadi milimita 50 na 30 kwa kipindi cha siku tatu zijazo.

Ripoti zaidi zinaashiria kuwa mafuriko ya mvua huenda yakashuhudiwa katika nyanda za chini, huku kaunti za lamu, kilifi , mombasa , kwale na Tanariver zikitarajiwa kuathirika pakubwa na hali hiyo.

Wakazi wanaoishi maeneo ya chini wametakiwa kuhamia maeneo ya miinuko ili kuepukana na maafa ya mafuriko.

Show More

Related Articles