HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wahadhiri wakabiliwa kwa kuzuia masomo chuoni Kenyatta

Polisi walilazimika kuwatawanya wahadhiri na wafanyikazi wa vyuo vikuu pale walipoandamana kuelekea chuo kikuu cha Kenyatta kuzuia masomo yasiendelee.
Viongozi wa muungano wa wahadhiri wa vyuo vikuu hata hivyo wamesisitiza kwamba mgomo ungalipo na kuwa tangazo la uongozi wa wanafunzi hiyo jana kwamba warejelee masomo halina uzito.
Wakati huo huo katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Wilson Sossion leo hii amezuiliwa kuingia kwenye afisi yake.

Show More

Related Articles