HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Chama cha ODM kuandaa mkao wa faragha Naivasha kutoa mwelekeo

Baraza kuu la chama cha ODM linatarajiwa kuandaa kikao cha faragha kesho mjini Naivasha kujadili undani wa mchakato wa maafikiano kutokana na makubaliano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama hicho Raila Odinga ya Machi tarehe tisa.
Katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna amepuuzilia mbali matamshi ya baadhi ya wanachama wa Jubilee hasa wandani wakuu wa naibu rais kwamba Raila anataka kutumia fursa hii kujenga msingi atakaoutumia kwenye debe la mwaka 2022.

Show More

Related Articles