HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Manaibu 4  wa chifu wajeruhiwa na washukiwa wa kulangua bangi

Polisi katika eneo la Gatundu kaskazini kaunti ya Kiambu, wanawasaka ndugu wawili waliowashambulia na kuwakata kwa upanga manaibu wanne wa chifu waliokuwa wameenda kumkamata mmoja wao kwa tuhuma za kuuza bangi.

Wakati wa tukio hilo mshukiwa mmoja anadaiwa kutoroka akiwa amefungwa pingu.

Naibu Kamishna wa Gatundu Fredrick Muli amesema kuwa kilo tano za bangi zilipatikana nyumbani kwa washukiwa.

Show More

Related Articles