BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Chikuzee Kukosa Katika Orodha Ya Wasanii 10 Bora Yazua Hisia Mseto.

Baada ya kikosi cha #MwakeMwake  kufanya utafiti wa kipekee na kuachia list ya wasanii 10 maarufu zaidi katika ukanda huu wa pwani hisia mseto zimeimbuka kutokana na list hiyo.

Baadhi Wasanii tulio zungumza nao wameonyesha kuridhishwa na Nafasi zao katika orodha hii.

Mmoja wa wasanii hao ni Msanii anaye kua kwa kasi zaidi kelechi Afrikana ambaye  amekubaliana na utafiti huo na kusema kua bidii yake ndio iliyo mfikisha katia upeo wa list hiyo na kuwashauri wasanii wengine kuwa na bidiina wenye Nidhamu.

Msanii mwenye uwezo mkubwa Ohmslaw Montana pia ameonyesha kufurahia nafasi yake  katika orodha hiyo.  Alikua na haya yakusema.

 

“MIMI NLIFEEL POA KUONA MSANII CHIPUKIZI KAMA MIMI NAEZA MAKE IT KWA TOP TEN ARTISTS  ITANISAIDIA KUTIA BIDII KABISA ILI KUPIGANIA NAFASI YANGU.”

 

Bawazir   pia hakuachwa nyuma na kuwaomba walio katika nafasi za juu kuwafungulia walio chini milango zaidi kwa kuwashirikisha katika collabo.

KUFIKA KATIKA TOP 5 NI HATUA NZURI KWANGU NAPIA NITTIA BIDII ZAIDI ILI KUPATA KATIKA NAFASI BORA ZAIDI LAKINI ITAKUA VYEMA KWA WALE WALIO JUU YETU KUSHIRIKIANA NASI

 

Aidha Producer TK2 ameyapinga matokeo haya na kuonekana akipigia upato Chikuzee. Producer huyo

amedai kuwa Chikuzee ni moja  ya wasanii wenye kipaji na uwezo wa hali ya juu na anafaa kuwa katika Nafasi ya tano Bora.

Show More

Related Articles