HabariMilele FmSwahili

Wanajeshi 7 wa KDF wauwawa baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi Dobley kwenye mpaka wa Kenya -Somalia

Wanajeshi saba wa KDF wameuwawa baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi kati eneo lililoko kati ya Dobley na Dagalema kwenye mpaka wa Kenya na Somalia. Katika taarifa jeshi la KDF wanajeshi wengine wawili waliojeruhiwa wamesafirishwa kwa ndege kupokea matibabu kaunti ya Wajir. Wanajeshi hao walikuwa wakisafiri kutoka Daadab kuelekea Dobley wakipitia Dagalema wakati gari lao aina ya Landcruiser lilipokangaya kilipuzi hicho na kuharibiwa vibaya. Kwa sasa jeshi limeanzisha msako dhidi ya washambuliaji wanaoaminika kuwa magaidi wa Al Shabbab

Show More

Related Articles