HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta akutana na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Rais Uhuru Kenyatta ameshauriana leo na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed katika ikulu ya Nairobi. Abiy ametunukiwa heshima ya mizinga 19 kando na kukagua gwaride la heshima alipowasili kwenye ikulu ya Nairobi. mkutano baina ya viongozi hao unanuia kuimarisha uhusiano wa karibu baina ya Kenya na Ethiopia. kadhalika rais Kenyatta na waziri mkuu Abiy wanatarajiwa kuangazia mikakati ya pamoja ya kukabiliana na ugaidi katika ukanda wa afika mashariki na kuyasaidia mataifa ya Sudan Kusini na Somalia kupata amani na uthadibiti. Kulingana na msemaji wa ikulu Manoah Esipisu uhusiano wa kibiashara pia utaangaziwa.

Show More

Related Articles