HabariMilele FmSwahili

Mbunge Mohamed Ali asema yuko tayari kuzika tofauti kati yake na gavana Joho

Mbunge wa Nyali Mohamed Ali sasa anasema yuko tayari kuzika tofauti zilizopo baina yake na gavana wa Mombasa Hassan Joho. Ali anasema yuko tayari kuiga mfano wa rais Kenyatta na Raila Odinga kushirikiana kwa manufaa ya taifa. Hata hivyo ameshikilia kuwa ataendelea kuikosoa serikali ya gavana Joho. Kati ya mengi ali anasema atahakikisha kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa haijihusishi katika ufisadi huku pia akiitaka kutatua tatizo la mrundiko wa taka kaunti hiyo.

Show More

Related Articles