HabariMilele FmSwahili

Wanachama wa kamati kuu ya ODM wakongamana mjini Naivasha

Wanachama wa kamati kuu ya chama cha ODM wanakongamana mjini Naivasha kwa mkutano wa siku mbili. Ni mkutano wa kwanza tokea kinara Raila Odinga alipoafikiana kufanya kazi na rais Uhuru Kenyatta. Raila anatarajiwa kutumia mkutano huu kujibu maswali ya wabunge kuhusiana na mwafaka huo. Aidha katika mkutano huo Raila anatarajiwa kufafanua zaidi kuhusu pendekezo lake la mageuzi ya katiba ili kubadilisha mfumo wa uongozi nchini. Hata hivyo kulingana na mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi mkutano huo hautatumika kujadili ODM kujiondoa kwenye muungano wa NASA.

Show More

Related Articles