HabariPilipili FmPilipili FM News
KMFRI Yazundua Kifaa Maalum Cha Kuvua Samaki Aina Ya Kamba Kamba.

Sekta ya Uvuvi wa samaki aina ya Kamba Kamba inatarajiwa kuimarika zaidi baada ya Tasisi ya Utafiti wa Bahari na Uvuvi Nchini KMFRI kuzindua Kifaa maalum cha kuwavua samaki hao.
Edward Kimani, mtafiti Mkuu kwenye Tasisi hiyo amesema Kifaa hicho kinauwezo wa kupunguza Uzito wa neti ya kuwavua samaki hao, hivyo kuziwezesha meli za uvuvi kutekeleza shughuli hiyo kwa urahisi zaidi.
Amesema kuwa Idara hiyo itaendelea kuushinikiza utawala wa Kimataifa unayosimamia uvuvi wa viumbe vya majini, (National Oceanic and Atmospheric Administration) NOAA kuidhinisha Utumiaji wa Kifaa hicho humu nchini hivyo kuiwezesha Sekta hiyo kupata masoko zaidi la kimataifa.