HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Ari na Ukakamavu: Mwanariadha gwiji anayeteleza kwenye theluji licha ya ulemavu

Kwenye makala ya Ari na Ukakamavu  hii leo tunaangazia safari  yake Daniel Safari kijana ambaye aliumwa na nyoka akiwa na umri wa miaka 5 na ili kuokoa maisha yake ikiwabidi madaktari kuukata mguu wake wa kulia.

Hata hivyo hilo halikumzuia kutambua na kukuza talanta yake.

Kwa sasa Daniel ndiye mkenya pekee ambaye anashiriki kwenye michezo ya walemavu ya kuteleza kwenye theluji, kwa kiingereza ni Skiing.

Mwanahabari wetu Kimani Githuku alijiunga naye kwenye uwanja wa michezo wa Kasarani ambapo anaendelea na mazoezi yake na kutuandalia taarifa ifuatayo.

Show More

Related Articles