HabariPilipili FmPilipili FM News

Shule Ya Fungwa Na Kugeuzwa Kambi ya Waathiriwa Wa Mafuriko Kilifi.

Masomo yanaendelea kuathirika kwa siku ya tano mfululizo katika Shule ya upili ya Garashi eneo la Magarini kaunti ya kilifi. Hii ni kufuatia shule hiyo kufungwa na kugeuzwa kambi ya mda kusaidia zaidi ya waathiriwa elfu 2 wa mafuriko.

Wanafunzi katika  shule hiyo wanasema madarasa yao yamegeuzwa kambi ya wahanga wa mafuriko, jambo ambalo wanahofia huenda likathiri maandalizi ya mitihani ya kitaifa.

Wanafunzi hao sasa wanataka serikali kutafuta mahala mbadala pa kuihamishia kambi hiyo ili kupisha shughuli za masomo kuendelea.

Show More

Related Articles