People Daily

Zaidi Ya Watu Mia Moja Wamefariki Kutokana Na Mafuriko Hapa Nchini

Takriban watu 112 wamefariki kote nchini kufikia sasa, huku familia elfu 48 zikiachwa bila makao, na zaidi ya wengine takriban elfu 30 wakiuguza majera madogo kutokana na mafuriko.

Kulingana na ripoti ya shirika la mslaba mwekundu zaidi ya mifugo elfu 20 imesombwa na mafuriko, huku ekari zaidi ya elfu 22 zikiharibiwa kabisa.

Ripoti zaidi inaeleza kuwa zaidi ya shule 100 zimeathirika na mafuriko kote nchini, 29 zikisombwa kabisa na maji, huku zaidi ya hospitali 42 pia zikiathirika.

Kufikia sasa jumla ya kaunti 32 kati ya zote 47 Zimeathirika na mafuriko zikiongozwa na Tanariver, Kilifi na Garisa.

 

Show More

Related Articles