HabariMilele FmSwahili

Moto uliozuka katika jumba la kibiashara la Sarit mtaani Westlands, Nairobi wadhibitiwa

Moto uliozuka katika jumba la kibiashara la Sarit mtaani Westlands hapa Nairobi umedhibitiwa. Usimamizi wa jumba hilo unasema moto huo unaodaiwa kuanzia katika orofa ya chini umeathiri zaidi orofa ya 2 jumba hilo. Maafisa wa zima moto na polisi wako katika eneo hilo. Chanzo chake bado hakijabainika. Hakuna majeruhi walioripotiwa. Watu wote wametakiwa kuondoka kwenye jumba hilo.

Show More

Related Articles