HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta kurejea shuleni Jumatatu ijayo

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta wametakiwa kurejea shuleni kufikia Jumatatu ijayo. Ni baada ya wahadhiri wao waliokuwa wakigoma kusaini nyaraka za kujitolea kurudi kazini huku matakwa yao ya nyongeza ya mishahara ikishughulikiwa na serikali. Baadhi ya vyuo vikuu vya umma vinaripotiwa kuwafuta kazi wahadhiri wake wanaogoma kufuata agizo la kurejea darasani.

Show More

Related Articles