HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakenya Wamtaka Raila Pia Kuomba Msamaha.

Wakenya sasa wanamtaka kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kufuata mkondo wa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kuwaomba msamaha wakenya , kwa chochote ambacho huenda alifanya kinyume na matarajio ya wananchi wakati wa siasa za mwaka jana.

Kulingana na taarifa kwenye vyombo vya habari baadhi ya wananchi wanahisi hatua hii itaendana na ushirikiano kati yake na rais Kenyatta ambao ulilenga kuunganisha wakenya.

Aidha wengine wanahisi hatua hii itatoa mwelekeo mzuri kwa amani ya wakenya kote nchini

Wengi wameonyesha kuridhia hatua ya rais Kenyatta kuwaomba msamaha wakenya wakati wa hotuba yake kwa taifa hasa kutokana na tofauti za kisiasa zilizoshuhudiwa baina ya mirengo ya Jubilee na NASA.

Show More

Related Articles