MichezoPilipili FmPilipili FM News

Sebastien Migne Ndiye Mkufunzi Mpya Wa Timu Ya Harambee Stars.

Shirikisho la soka nchini FKF limemzindua rasmi mkufunzi mpya wa timu ya taifa harambee stars hii leo jijini Nairobi.

Sebastien Migne kutoka Ufaransa amezinduliwa na shirikisho hilo katika kikao na waandishi wa habari pamoja na rais wa shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa.

Migne anachukua nafasi ya Mbelgiji Paul Put ambaye aliachia ngazi.

Tuna uhakika na uwezo wake wa ukufunzi na anaijua Afrika vizuri na hio itakua rahisi kwake kuipeleka Kenya katika mashindano makubwa ulimwenguni”. Amesema  Mwendwa.

Kwa upande wake mkufunzi huyo amesema anafuraha kubwa kupata fursa kuifunza Kenya na yuko tayari kwa changamoto mpya  na ameahidi kuhakikisha kuwa anazunguka katika mechi za ligi kuu humu nchini kutazama vipaji vya wachezaji.

Migne ambaye amempiku Mholanzi Ruud Krol amekuja na naibu wake ,mkufunzi wa makipa na mtu wake wa maswala ya matibabu

Sebastien Migne ameshawahi kuwa naibu mkufunzi wa timu ya taifa ya Togo katika mashindano ya bara afrika 2017 na naibu mkufunzi wa taifa la Congo mwaka 2015.

Kazi yake kubwa ya kwanza ni kibarua dhidi ya Ghana kusaka nafasi yakuelekea kombe la bara Afrika Septemba 7 mwaka huu hapa nchini

 

 

Show More

Related Articles