HabariMilele FmSwahili

Mtoto wa miaka 3 afanyiwa upasuaji baada ya kupatikana na sindano 7 mwilini Pokot Magharibi

Madaktari huko Kapenguria wamemfanyia upasuaji mtoto wa miaka 3 aliyepatikana na sindano 7 mwilini .Hii ni baada yake kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Kapenguria kaunti ya Pokot Magharibi. Picha za xray zilionyesha sindano 5 zikiwa tumboni na mbili zikiwa kwenye mgongo. Madaktari wanasema huenda sindano hizo zilidungwa mwilini mwa mtoto huyo na kuwa hakuzimeza.afisa wa afya kaunti hiyo Ibrahim Longolomoi anasema wamepiga ripoti kwa polisi ili uchunguzi uanzishwe.

Show More

Related Articles

Check Also

Close