HabariPilipili FmPilipili FM News

Sossion Asistiza Kutobanduka Kama Kiongozi Wa KNUT.

Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini Knut Wilson Sossion asema ataendelea na majukumu yake  kama  msemaji wa chama hicho licha ya kusimamishwa kazi .

Katika kikao na waandishi wa habari Sossion amesema  kuwa kulingana na sheria yeye ndiye msemaji halali  na kuwaonya wanaopinga utenda kazi wake kuwasilisha kesi yao kwa kongamano la wajumbe la kila mwaka.

Jumatano,tofauti ya muungano huo zilijitokeza wazi pale Sossion alipofika pekeyake kwenye mkutano na mwajiri wa walimu kuhusu kupandisha vyeo.

Viongozi wengine wakiongozwa na kaimu katibu mkuu Hezbon Otieno hawakufika,wakidai kuwa waliomba kuhairishwa kwa mkutano ili kupewa nafasi kusuluhisha mvutano uliopo.

Sossion alitolewa madarakani jumatatu wiki hii na wanachama wa bodi kuu ya kitaifa ili aweze kushughulikia majukumu yake kama mbunge mteule.

 

 

Show More

Related Articles