HabariPilipili FmPilipili FM News

KWS Yahimizwa Kuthibiti Wanyamapori Tana Delta.

Wakazi wa Tana Delta kaunti ya Tana River sasa wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa na wanyamapori.
Wakiongea na meza yetu ya habari wakazi hao wanasema siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la visa vya wanyama kushambulia wananchi , hali ambayo wameitaja kuchangiwa na mafuriko yanayoshuhudiwa eneo hilo.

Abae ametoa changamoto kwa shirika la hifadhi ya wanyamapori nchini KWS kuweka mikakati ya kuthibiti wanyama kama vile kiboko na mamba, pamoja na kuhamasisha wananchi jinsi ya kujikinga dhidi ya wanyama hao.

Show More

Related Articles