HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Yahimizwa Kuongeza Nguvu Kupigana Na Ufisadi.

 

Serikali imetakiwa kutoa ushirikiano kwa taasisi zote za humu nchini ili kuzipa nguvu ya kufanya kazi zao kwa njia huru kama inavyotakiwa katika katiba.

Akitoa wito huu mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binaadamu la Muhuri Hassan Abdile amesema endapo hakutakuwa na vitendo katika maneno ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga basi ushirikiano wao hautakua na manufaa kwa wakenya.

Abdile aidha amemtaka rais Uhuru Kenyatta kushirikiana na viongozi wote wa kisiasa katika kuhakikisha wanapigana na ufisadi.

 

 

 

 

Show More

Related Articles