HabariPilipili FmPilipili FM News

Waathiriwa Wa Mafuriko Wapewa Mipira ya Kondomu Kilifi.

Wizara ya afya ya kaunti ya Kilifi imetoa mipira ya kondomu 3,000 kwa waathiriwa wa mafuriko katika kambi ya Garashi eneo hilo.

Katika  taarifa kwa vyombo vya habari katibu wa Afya katika kaunti hiyo dakitari Anisa Omar, amesema pia wameongeza huduma za afya kwa waathiriwa wa mafuriko ambao wako katika kambi hiyo ya mda.

Kulingana naye takriban Wakazi 6,000 ambao ni waathiriwa wa mafuriko mjini Malindi waliomba wasambaziwe mipira ya kondomu, wakisema itawasaidia kukabiliana na hofu ya kupata magonjwa kama vile Ukimwi.

Show More

Related Articles