HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Rais awaomba msamaha aliowakosea wakati wa uchaguzi 2017

Kwenye hotuba yake ya kwanza tangu kuchaguliwa kwa kipindi cha pili, Rais Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha wakenya ambao kwa njia moja au nyingine aliwakosea hasa wakati wa kura za mwaka jana na kuweka bayana sababu kuu za yeye na Raila Odinga kuafikiana kwa ajili ya mapenzi yao kwa taifa na wakenya kwa jumla.

Kenyatta amewataka viongozi wote hasa wanasiasa kuzingatia umuhimu wa kuhubiri amani, utangamano na umoja wa kitaifa, huku akiwataka wakenya kubadili mkondo wa kuendesha siasa nchini na hasa kukemea vikali misimamo ya kikabila ambayo huligawanya taifa msimu wa siasa za uchaguzi unapobisha hodi.

Show More

Related Articles