BiasharaMilele FmSwahili

Kenya power yaahidi kuangazia lalama zilizoibuliwa na wakenya kuhusu huduma zake

Kampuni ya Kenya Power imeahidi kuangazia lalama zilizoibuliwa na wakenya kuhusu huduma zake kufikia saa nane alasiri Ijumaa. Meneja mkurugenzi wa Kenya power Ken Tarus ametetea kampuni hiyo akisema wamekuwa waaminifu kwa wateja wake na kukana madai ya kuweka ada za umeme ambazo hazistahili. Tarus anasema hakuna huduma za umeme zitakakatizwa kutokana na kufeli kwa mitambo ya trans foma wakati wa mvua. Anasema viwango vya maji pia katika mabwawa 7 ya kuzalisha umeme pia vimeimarika.

Show More

Related Articles