HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya shule 50 kaunti ya Tana River zakosa kufunguliwa kutokana na mafuriko

Zaidi ya shule 50 huko Tana River zingali zimefungwa na maji ya mafuriko na kukosa kufunguliwa. Kamanda wa polisi eneo la Pwani Noah Mwivanda anasema eneo la Tana River lingali limeathirika na mafuriko yaliyosababishwa na mvua inayonyesha. Anasema baadhi ya familia zimeachwa bila makao eneo la Tana River Kaskazini kijiji cha Kilelengwani. Anasema wanaweka mikakati ya kuhakikisha wenyeji wanahamia maeneo salama na kupungua maafa yanayotokana na mvua hiyo.

Show More

Related Articles