HabariPilipili FmPilipili FM News

Mvua Yatatiza Masomo Taita Taveta.

Huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini baadhi ya wanafunzi katika maeneo ya Abori na kiwalwa eneo bunge la Taveta kaunti ya Taita Taveta wanaendelea  kuathirika kimasomo.

Kulingana na afisa mkuu wa elimu eneo bunge la Taveta,Hassan Abdurahman,madarasa katika maeneo hayo yamejaa maji huku baadhi ya majumba yakiwemo vyoo yakibomoka kutokana na mafuriko ya mvua.

Aidha afisa huyo anasema jumla ya walimu wakuu 16 pia wamepewa uhamisho eneo hilo hadi kaunti za makueni na kajiado, suala ambalo anadai litasaidia walimu kuimarisha viwango vya elimu shuleni.

Show More

Related Articles