HabariPilipili FmPilipili FM News

Usalama Waimarishwa Katika Majengo Ya Bunge Wakati Rais Akitarajiwa Kuhutubia Taifa.

Usalama umeimarishwa katika majengo ya bunge jijini Nairobi kabla ya hotuba ya rais Kwa taifa badae adhuhuri ya leo.

Rais ameratibiwa kuhutubia taifa katika kikao maalum ambacho kitajumuisha wajumbe wa bunge la kitaifa na lile la senate.

Wakati wa kikao hicho rais anatarajiwa kuweka wazi ajenda za ushirikiano wake na kinara wa chama cha ODM Raila odinga.

Aidha rais pia anatarajiwa kueleza mipango ya serikali ya jubilee katika muhula wake wa pili na wa mwisho, ikiwemo kufafanua zaidi kuhusu ajenda nne kuu za serikali ya jubilee, ambazo ni afya bora kwa wote, uzalishaji wa bidhaa kwa wingi, Nyumba za nafuu kwa wananchi na uslama wa chakula.

Mengine yanayotarajiwa kupewa kipao mbele ni usalama wa Taifa, pamoja na mwafaka wa kuunganisha wakenya.

Show More

Related Articles