HabariMilele FmSwahili

Rais atangaza nyongeza ya 5% kwa mishahara ya wafanyikazi wa chini nchini

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza nyongeza ya asilimia tano kwa kiwango cha chini ya mishahara ya wafanyikazi wa taifa. Kwenye hotuba yake iliosomwa na waziri wa leba Ukur Yattani wakati wa sherehe za kusherehekea siku ya wafanyikazi duniani, Rais Kenyatta ameagiza nyongeza hiyo kutekelezwa mara moja na waajiri wote. Licha ya kuwepo pingamizi kutoka kwa waajiri dhidi ya kutolewa nyongeza ya mishahara kutokana na kile walidai ni kuzorota kwa uchumi wa taifa,rais amesema lazima maslahi ya wafanyikazi yaangaziwe kwa mujibu wa kauli mbiu ya mwaka huu.

Rais ametumia sherehe hizo kuelezea jinsi taifa limeathirika kutokana na migomo ya mara kwa mara ya wafanyikazi wa sekta za umma akitaka lalama zote kutatuliwa kupitia majadiliano. Rais amesema sio lazima kuwepo migomo ili lalama za wafanyikazi zitatuliwe hivyo haja ya kuwepo mazungumzo baina ya wafanyikazi na mwjairi wao.

Rais amevitaka vyama vya wafanyikazi kuisaidia serikali kutatuza changamoto zinazowakumba wafanyikazi badala ya kuwa mstari wa mbele kushtumu na kuitisha migomo anayosema haileti faida yeyote kwa wakenya wala kwa ukuaji wa taifa.

Show More

Related Articles