HabariMilele FmSwahili

Sherehe za kitaifa za Leba zafanyika katika bustani ya Uhuru, Nairobi

Waziri wa leba Ukur Yattan, kinara wa ODM Raila Odinga, kinara wa ANC Musalia Mudavadi, katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli ni baadhi ya viongozi ambao tayari wamewasili katika bustani ya Uhuru hapa Nairobi kuhudhuria sherehe za kitaifa za leba. Aidha viongozi wa miungano tofauti ya wafanyikazi wanaongoza sherehe hizo katika kaunti zote 47 nchini. Ni sherehe ambazo hotuba zake zitashamiri mabadiliko yaliopendekezwa na wizara ya Leba kufanyia mageuzi vipengee kadhaa katika sekta za uajiri wa umma.

Show More

Related Articles