HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakware Babies Si Kikundi Cha Uhalifu Wasema Polisi Mombasa.

Uchunguzi uliofanywa na idara ya usalama kaunti ya Mombasa umebainisha kuwa kikundi cha wasichana maarufu kama wakware babies kinachodaiwa kusumbua kwa kupokonya wanawake mabwana zao eneo la Bombolulu si moja wapo ya makundi hatari yanayohusishwa na utovu wa usalama.

Akiongea na meza yetu ya habari kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara ameweka wazi kikundi hicho cha wasichana wa umri kati ya 13 hadi 17 ni kikundi kinachojihusisha na kujiuza miili yao huku akionya wanaume wanaohusika kimapenzi na wasichana hao watachukuliwa hatua kali za kisheria kwani amewataja wasichana hao kuwa wadogo.

Wakati huohuo Ipara amewaonya vikali wazazi wanaowaachilia watoto wao wadogo kujiingiza katika biashara ya kujiuza miili yao ili wapate lishe.

 

Show More

Related Articles