HabariPilipili FmPilipili FM News

Wilson Sossion Asimamishwa Kama Katibu Wa KNUT.

Chama cha walimu nchini KNUT kimemsimamisha Katibu mkuu wa chama hicho Wilson Sossion akisubiri uchunguzi wa kina kuhusu mienendo yake.

Uamuzi huo uliafikiwa jumatatu kufuatia mkutano wa baraza kuu la kitaifa la walimu NEC, ambapo wanachama 22 walipiga kura dhidi ya hoja ya kujadili mienendo ya Sossion.

Mamlaka kuu ya chama cha KNUT kwa sasa imemteua naibu katibu mkuu Hesbon Otieno kama kaimu katibu mkuu wa mda mfupi, ili kushikilia uendeshaji wa shughuli za walimu.

Badae wanachama wa baraza kuu la walimu NEC wanatarajiwa kukutana kujadili hatma yake Sossion.

Show More

Related Articles