HabariPilipili FmPilipili FM News

Bodi Yakuratibu Ubora Wa Filamu Yatoa Onyo Kwa Wenye Kubandika Mabango Yanayokiuka Maadili.

Kampuni zinazotangaza kupitia mabango zimeonywa kuwa mabango yao yataondolewa endapo yatapatikana na picha zinazokiuka  maadili.

Hayo ni kwa mujibu wa afisa mkuu wa bodi ya kuratibu ubora wa filamu nchini, KFCB eneo la pwani Boniveture Kioko, ambaye anasema, kabla tangazo liangikwe kwa bango, lazima lipitie kwa bodi hiyo, kukaguliwa na kuidhinishwa.

Wakati huohuo kioko ametoa makataa ya masaa 24 kwa walio na mabango ambayo yanakiuka maadili, kuyatoa kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao

Haya yanjiri siku chache tu, baada ya mamlaka kuu ya bodi hiyo kupiga marufuku filamu moja ya humu nchini kwa jina ‘’Rafiki’’baada ya filamu hiyo kudaiwa kuchochea mapenzi ya jinsia moja.

 

 

 

 

Show More

Related Articles