HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Maafisa wa KFS wadaiwa kutoa leseni bandia za ukataji miti

Shirika la huduma za misitu nchini KFS limelaumiwa pakubwa kwa uharibifu wa misitu kote nchini.

Kwenye ripoti iliyowasilishwa na jopo lililoundwa kubaini tatizo la upungufu wa misitu, viongozi wa KFS walihusika kwa njia kadhaa kutoa leseni bandia za ukataji miti na kisha kukosa kuweka mikakati thabiti ya kulinda misitu dhidi ya wakataji miti kiholela.

Naibu Rais William Ruto ambaye alipokea ripoti hiyo pamoja na Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko walisema mapendekezo kwenye ripoti hiyo yatatekelezwa kikamilifu hivi karibuni.

Show More

Related Articles