HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Kuchimba Visima 2,419 Kukabiliana Na Kiangazi.

Jumla ya visima 2,419 vinatarajiwa kuchimbwa kote nchini kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2018, ikilinganishwa na visima 1,557 vilivyo chimbwa mwaka jana katika juhudi za kukabili hali ya kiangazi.

Mpango huo ambao unaendeshwa na wizara ya maji na unyunyuziaji pia  unatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa maji safi kwa wananchi hasa kaunti za Kilifi, Taita-Taveta na Kwale.

Wakati huo huo utafiti wa idara ya Takwimu nchini unaonyesha kuwa kiwango cha ardhi iliyo na misitu ambayo ni mojawapo ya vyanzo vya maji nchini imeongezeka kutoka ekari milioni 4.1 mwaka wa 2016, hadi ekari milioni 4.2 mwaka uliopita wa 2017.

Show More

Related Articles