HabariMilele FmSwahili

Jopo :KFS inafaa kuwajibikia uharibifu mkubwa wa misitu unaoshudiwa nchini

Usimamizi wa shirika la misitu nchini KFS unafaa kuwajibikia uharibifu mkubwa wa misitu ulioshudiwa nchini. Kulinga na jopo lililotwikwa jukumu la kutathmini mbinu za kuokoa misitu, shirika la KFS limesheheni ufisadi na uzembe wa baadhi ya maafisa. Akiwasilisha ripoti ya jopo hilo kwa naibu rais William Ruto mwenyekiti Marion Wakanyi Kamau amesema swala la uvamizi wa misitu kinyume na sheria limetokana na wasimamizi wa KFS kutokuwa na uadilifu. Naye naibu rais William Ruto ametoa hakikisho kuwa mapendekezo ya ripoti hiyo itakayowasilishwa kwa rais siku 10 zijazo yatatekelezwa kikamilifu. Ruto pia amedokeza kuwa serikali itatumia mashirika ya KFS na NYS kupanda miti zaidi nchini.

Show More

Related Articles