HabariPilipili FmPilipili FM News

Kamati Ya Uwiano Iliyoteuliwa Na Rais Kenyatta Na Odinga Kuanza Majukumu Karibuni.

Kamati ya washauri 14 wanaotarajiwa kuongoza mazungumzo ya kitaifa kufuatia ushirikiano wa Rais Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga sasa inatarajiwa kuanza majukumu yake hivi karibuni.

Kati ya waliojumuishwa ndani ya kamati hiyo ni seneta wa Busia Amos Wako, seneta wa Garisa Yusuf Haji, Adams Oloo, Agness Kavindu, Flourence Omose, Saeed Mwangumi pamoja na James Matundura.

Aidha kamati hiyo inaongozwa na Martin Kimani na mwenzake Paul Mwangi lengo kuu ikiwa ni kuongoza mchakato wa kuleta maridhiano nchini, hasa kutokana na mgawanyiko mkubwa ambao ulitokana na chaguzi za mwaka jana.

Show More

Related Articles