HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanafunzi Akufa Maji Kwale.

Mwanafunzi mmoja mwenye umri wa miaka 25 ameripotiwa kufa maji  katika fuo ya bahari ya sawasawa huko Msambweni kaunti ya Kwale.

Marehemu kwa jina Nickson Kipchumba ambaye alikuwa mwanafunzi katika chuo cha mafunzo ya udaktari  cha Msambweni ,alikutana na mauti  yake wakati akiogelea na wenzake wawili.

Akithibitisha tukio  hilo  naibu kamishna wa msambweni  Ronald  Enyakasi,  anasema polisi walipata habari za kupotea kwa mwanafunzi huyo mwendo wa saa tisa mchana,  na kuanzisha juhudi za kuusaka mwili wake, kabla ya kuupata badae  saa kumi na mbili jioni .

Kwa ssa Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali kuu ya  Msambweni.

Show More

Related Articles