HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Naibu wa rais azuru Kericho, Raila apeleka siasa za uwiano Kajiado

Viongozi wa chama cha ODM sasa wanamshtumu naibu wa Rais William Ruto kwa kupinga kuandaliwa kwa kura ya maoni ili kurekebisha katiba.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa chama cha chungwa Edwin Sifuna na Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed viongozi hawa wamemtaja Ruto kama kiongozi anayepinga uwiano huku wakimtaka kukaa kando na kuwapa nafasi wanaounga mkono kura ya maoni kusonga mbele.
Hata hivyo, Ruto amesema kuandaa kura ya maoni ni kuinyima serikali ya Jubilee nafasi ya kutekeleza ahadi zake kwa wakenya, kwani itawalazimu wananchi kurejea kwenye awamu nyingine ya kampeini.

Show More

Related Articles