HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Watu 4 waangamia katika maporomoko, Murang’a

Watu wanne wa familia moja wameangamia baada ya maporomoko ya ardhi kusomba nyumba zao katika kijiji cha Inoi huko Kahuro, kaunti ya Murang’a.

Katika kaunti ndogo jirani ya Mathioya eneo la Gitugi, maporomoko hayo yalisomba nyumba kadhaa na hata daraja la iyego na kufikia sasa shughuli ya kumsaka mtu mmoja aliyekwama chini ya vifusi bado inaendelea.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa bado inasisitiza kuwa kati ya usiku wa leo hadi kesho saa tatu usiku kuna maeneo mbalimbali ambayo yatapata mvua kubwa.

Show More

Related Articles