HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

KDF wasaidia kuwaokoa wenyeji Kilifi walioathiriwa na mafuriko

Maelfu ya wakaazi kutoka kaunti za Kilifi na Tana River wamebaki bila makao, mavazi na hata chakula baada ya mafuriko kuzidi katika maeneo hayo.
Wanajeshi wa KDF kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Kilifi walianza oparesheni ya kuokoa wakaazi hao walioathirika zaidi.
Aidha idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini imetahadharisha wakazi katika maeneo ya Pwani hasa Lamu, Kilifi, Kwale na Tana River kuhusu kuwepo mvua itakayokuwa ya kiwango cha juu zaidi kuanzia hapo kesho hadi wiki ijayo.

Show More

Related Articles