HabariMilele FmSwahili

Rais atoa changamoto kwa nchi za Afrika kuboresha mfumo wa elimu

Rais Uhuru Kenyatta ametoa changamoto kwa nchi za Afrika kutatua tatizo la idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawahudhurii masomo. Rais anasema nchi za bara hili zinapaswa kuangia upya malengo yao na kuboresha mifumo ya kutoa elimu.

Akifunga kongamano la mawaziri wa elimu kutoka Afrika hapa jijini Nairobi rais anasema kufikia sasa ni nchi saba pekee za Afrika zimeafikia malengo ya kuhakikisha kuwa kila mtoto anaweza kujiunga na shule ya msingi jambo analosema linapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano.

Amesisitiza umuhimu wa raia wa Afrika kuelimika ipasavyo ili kushiriki kikamilifu katika kutatua changamoto mbali mbali zinazolikumba bara hili.

Show More

Related Articles